KUHUSU COLD FARM LOGISTICS

Ubora, Usafi na Delivery ya Uhakika

Tunawafikishia familia na biashara za Arusha bidhaa bora za kuku kwa huduma inayoweza kuaminika.

HADITHI YETU

Karibu Cold Farm Logistics

Cold Farm Logistics Limited ni kampuni ya Kitanzania inayojishughulisha na uzalishaji, uchakataji na usambazaji wa bidhaa bora za kuku, ikiwa na dhamira ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata protini bora, salama na yenye bei nafuu.
Safari yetu ilianza kwa kufuga kuku wa kisasa 500 pekee mwaka 2023. Leo, kampuni imekua na kuzalisha maelfu ya kuku kila mwezi, ikijenga mfumo wa kisasa unaojumuisha ufugaji, uchinjaji, uchakataji na usambazaji wa bidhaa za kuku zenye ubora wa hali ya juu.
Kupitia chapa yetu ya KUKUGOLD, tunaleta suluhisho la kisasa kwa mahitaji ya familia za Kitanzania. Bidhaa yetu ya KUKUGOLD Smoked Chicken hutayarishwa kwa kutumia moshi wa asili, hivyo kuhifadhi ladha halisi ya kuku na kuongeza muda wa kuhifadhi bila kupoteza ubora wake. Bidhaa hii imekusudiwa kuwasaidia watu wenye shughuli nyingi kupata chakula kitamu, salama na rahisi kuandaa, huku ikichangia upatikanaji wa protini kwa gharama nafuu.
Aidha, tunazalisha KUKUGOLD AkDud (Chicken Powder) kiungo maalumu cha unga wa kuku kilichoboreshwa kwa tangawizi, kitunguu saumu na viungo vingine vingi vya asili ili kuongeza ladha ya vyakula kama pilau, maharage, mchuzi, mboga mboga na mapishi mengine mengi. Mbali na kuboresha ladha, bidhaa hii huongeza thamani ya lishe kwa kutumia viambato vya protini vinavyotokana na nyama ya kuku.

Dhamira Yetu

Kufikisha bidhaa za kuku salama, safi na zenye ladha bora kwa wakati.

Maono Yetu

Kuwa mshirika anayeaminika zaidi wa kuku na cold-chain delivery Arusha.

MCHAKATO WA UBORA

Tunatunza Ubora Katika Kila Hatua

Ukaguzi

Bidhaa huchaguliwa na kukaguliwa.

Usafi

Maandalizi hufuata viwango vya usalama.

Cold Chain

Joto salama huhifadhi freshness.

Delivery

Oda hufikishwa kwa wakati.

Tunawahudumia Nani?

Hoteli, migahawa, bars, lodges, catering, wauza chips, retailers, taasisi na familia zinazothamini ubora.

Hospitality

Retail

Nyumbani

Taasisi

Tuwe Mshirika Wako wa Usambazaji